Blac Chyna na Tyga waburuzana mahakamani kisa mtoto

Blac Chyna na Tyga waburuzana mahakamani kisa mtoto

Mwanamitindo kutoka nchini Marekani, Blac Chyna amfikisha mahakamani baba mtoto wake Tyga, ili apate haki ya malezi ya mwanaye.

Inaelezwa kuwa tangu wawili hao watengana Blac Chyna amekuwa akinyimwa haki ya kumuona na kuwasiliana na mtoto wao King mwenye umri wa miaka kumi ambaye anaishi na baba yake.

Blac Chyna amedai kuwa hafahamu afya ya mtoto huyo, anapoishi na hata shule anayosoma, kutokana na kesi hiyo imemlazimu Blac Chyna kuuza bidhaa zake za nguo na mikoba kwa bei ya hasara ili apate pesa za kuiendesha.

Hata hivyo mahakama bado haijaamua nani atashinda katika kesi ya wanandoa hao wazamani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags