Binti abadilisha muonekano mara 20 ili afanane na paka

Binti abadilisha muonekano mara 20 ili afanane na paka

Waliosema kuishi kwingi kuona mengi, hakika walikuwa na maana kubwa, kwani kuna baadhi ya vitu ambavyo waweza dhani ni ngumu kufanyika lakini kutokana na maendeleo ya sayansi, wapo binadamu wanaojaribu kuvifanya, kama ilivyo kwa baadhi ya watu kutumia njia mbalimbali za kisayansi kubadili mionekano yao na kuwa tofaui kabisa na walivyokuwa mwanzo.

Achana na wale wanaoenda kuongeza maumbo ya miili yao au wale wa kupunguza maumbo yao, yupo huyu binti wa miaka 22 raia wa Italia anayeitwa Chiara Dell'Abate maarufu kama Aydin Mod, yeye anafanya mabadiliko ya mwili wake ili aonekane kama paka binadamu.


Aydin Mod alianza kupenda na kufanya urekebishaji wa mwili tangu akiwa na umri wa miaka 11 ambapo alitoboa mwili wake kwa mara ya kwanza, lakini hadi kufikia mwaka huu tayari ametoboa mwili wake mara 72, na amefanya mabadiliko makubwa ya mwili mara 20 huku ulimi wake akiwa ameugawanyisha kati, ametoboa midomo ya juu kwa cm 0.8.


Ameweka vipandikizi 10 chini ya ngozi ya mikononi yake na kwenye paji la uso wake, amebadilisha mboni za macho yake kwa kuzichora tattoos, ameweka matobo pembezoni mwa pua, na amebadili kope zake. Katika moja ya mahojiano binti huyo alisema kuwa paka ni sahihi zaidi kwake kwani amekuwa akipenda wanyama hau na anadhani akiwa na muonekano wa paka atakuwa jasiri zaidi.


Hata hivyo alidai kuwa bado taendelea kufanya marekebisho zaidi ya wili wake ili aonekane zaidi kama paka binadamu na ili aweze kutimiza ndoto yake hilo alisema kuwa atatakiwa kufanya marekebisho zaidi kwenye macho yake, kukatwa midomo ya juu, na atatakiwa kuweka kitu kiitwacho transdermal, ambacho ni kama ngozi ndogo ili kupachika mkia.


Katika mabadiliko hayo alisema huwa na maumivu lakini anaamini maumivu ni ya muda mfupi na wala siyo jambo kubwa kwake, kwani kufanya mabadiliko hayo ya mwili wake kunamfanya ajisikie huru,na wala hajali watu wanafikiria nini juu yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags