Bill hulipwa pesa afichue siri za marehemu wakati wa mazishi

Bill hulipwa pesa afichue siri za marehemu wakati wa mazishi

Dunia ina mengi sana na kila mtu hutafuta njia ya kujipatia kipato ili mkono uende kinywani, wakati wewe umekaa bila kazi na kusema hakuna ajira, wala hauna mtaji wa kufanya biashara ili ujikwamue kimaisha fahamu kuwa kuna mtu ambaye kabuni mbinu ya kujipatia kipato kwa kutunza siri na kutoa siri za marehemu.

Wahenga walisema kufa kufaana, sasa basi vifo vya watu wengine vyamfaa mwanaume mmoja kutoka Australia anayefahamika kwa jina la Bill Edgar ambaye amejizolea umaarufu na kujipatia kipato kwa kutunza siri za watu na kisha kuzitoa baadaye kwa familia baada ya mtu huyo kufariki.



Inafahamika kuwa kuna siri ambazo mtu yeyote hatamani watu wengine wazifahamu kumuhusu yeye, lakini kupitia Bill unaweza kuitunza na kisha baadaye akaisimulia kwa familia na marafiki wakati wa mazishi yako.

Bill Edgar ni mwanaume kutoa Australia, ambaye pia ni muandishi wa vitabu na mshauri amebuni njia ya kujipatia kipato kwa watu kumsimulia siri zao ambazo hawakutaka zifahamike wakiwa hai, hivyo basi Bill huzitunza na kisha baadaye huzisimulia wakati wa mazishi endapo mtu huyo atafariki, katika moja ya interview aliyowahi kufanyiwa Bill alieleza kuwa anajipatia wateja wa kila aina ikiwemo wale ambao ni wagonjwa waliopo kitandani, na wengine ni wazima wa afya, humtafuta ili wapate huduma hiyo ya kutoa siri zao.

Anaeleza kuwa biashara yake imevuka mipaka kwani anapata wateja hadi kutoka nje ya nchi, watu humuomba asikilize siri zao ambao wameshindwa kuzitoa kwa watu wengine huku wakimtaka azitoe siku ambayo watafariki dunia.

Kazi ya kutunza siri za watu alianza mwaka 2018 baada ya rafiki yake kumpa siri na kisha kumuomba aisimulie siku akifaiki, ndipo Bill akaona kuwa wapo watu wenye vitu katika mioyo yao, wanashindwa kuvitoa hivyo sio vizuri kama watazikwa na siri hizo hivyo basi akaamua kuanza huduma hiyo kwa kuwatoza watu kwanzia milioni 5 hadi milioni 25.

Bill anadai kuwa hakuna mtu ambaye huomba apunguziwe bei kwani wengi hutambu kuwa wakifariki hawaendi na hizo pesa hivyo basi hulipa bila kusita huku akidai kuwa hadi sasa anasiri nyingi za wateja ambao anasubiri wafariki ili azitangaze kwenye misiba yao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags