Bila Maguire Man United hawatoboi

Bila Maguire Man United hawatoboi

‘Rekodi’ zinaonesha kuwa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited imekuwa ikishinda sana ‘mechi’ ambazo beki wao wa kati #HarryMaguire akianza kwenye kikosi cha kwanza.

Kwa mujibu wa Sky Sports, inaeleza kuwa tangu October 22 mwaka jana  katika ‘mechi’ 16 ambazo Man United ilianza ikiwa na beki huyo imeshinda ‘mechi’ 15, huku ‘mechi’ 44 ambazo ilianza bila ya mchezaji huyo  ilishinda ‘mechi’ 22 tu.

Vilevile Man United huwa na asilimia 93 ya kushinda kwenye mchezo wakati mchezaji huyo anapokuwa uwanjani.

Kwa upande wa kuruhusu mabao Man United ina wastani wa 0.7 wa kuruhusu bao katika ‘mechi’ ambazo Maguire ameanza na zile ambazo hakuanza ni wastani wa 1.3.

Mchezaji huyo alisajiliwa na ‘timu’ hiyo mwaka 2019 akitokea ‘klabu’ ya #LeicesterCity.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags