Bifu la Kim na Taylor laanza upya

Bifu la Kim na Taylor laanza upya

Album mpya ya mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Taylor Swift iitwayo ‘The Tortured Poets Departmen’ imeripotiwa kuwa nyimbo moja ambayo imemuongelea mfanyabiashara Kim Kardashian.

Kwa mujibu wa tmz imeeleza kuwa album hiyo inayotarajiwa kuachiwa siku ya leo wimbo uitwao ‘thanK you aIMee’ umedaiwa kuwa ni dongo kwenda kwa Kim kutokana na herufi kubwa zilizokuwepo kwenye jina la wimbo huo zinazotajwa kuwa jina la Kim (KK).

Endapo ngoma hiyo itakuwa ni dongo kwenda kwa Kim basi Swift atakuwa hajamaliza ugomvi wake na mfanyabiashara huyo.

Ikumbukwe kuwa bifu la Kim na Swift lilianza mwaka 2016 baada ya aliyekuwa mume wa Kim, Kanye West kutoa wimbo wa ‘Famous’ uliokuwa ukieleza kuwa Kanye ndiyo amefanya Taylor kuwa maarufu huku ikidaiwa kuwa Kim alihusika katika uandishi wa ngoma hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags