Bibi ajioa mwenyewe baada ya kukaa miaka 40 bila ndoa

Bibi ajioa mwenyewe baada ya kukaa miaka 40 bila ndoa

Nyie nyie, ama kweli ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni, basi bwana bibi mmoja kutoka nchini Marekani alifahamika kwa jina la Dorothy Fidel akiwa na miaka 77, ameamua kujioa mwenyewe baada yakuishi miaka 40 bila kua na mwanaume.

Mwanamama huyo hapo awali aliolewa na kudumu kwenye ndoa kwa miaka 9 kisha kupewa talaka jambo ambalo alijiapisha kua hatataka kua na mahusiano kamwe.Dorothy amesema aliwaza jambo gani anaweza kujifanyia lakumpa furaha hivyo akaona ni bora ajioe mwenyewe, anasema hakuwaza kama atapendeza kwenye nguo za harusi kiasi hicho na anajihisi mwenye furaha zaidi.

Kulingana na ripoti ya Today.com siku ya Jumanne, lilieleza kuwa Dorothy Fideli, maarufu kama Dottie alifunga ndoa Mei 13, ambapo ndoa hiyo ilihuzuriwa na majirani na ndugu zake.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post