Biashara zinazoweza kukuingizia sh 1milioni kwa mwezi

Biashara zinazoweza kukuingizia sh 1milioni kwa mwezi

Na Aisha Lungato

Niaje niaje watu wangu wa nguvu, i hope mko pouwa kabisa, kama ilivyoada kila wiki tunawasogezea vitu adimu katika anga za biashara, mada ya leo kila mtu itamkosha kwa aina yake.

Kama tunavyojua mitaani kuna biashara nyingi za kufanya ambazo zinatuingizia kipata ambacho tunakitumia kwa ajili ya matuminzi ya kila siku.

Bila kupoteza muda nimewasogezea mawazo ya biashara ambazo unaweza kuzifanya na zikakuingizia mkwanja mrefu endapo utakuwa na mzunguko mkubwa wa watu na uchangamfu wako

        Biashara ya kuuza bidhaa za nafaka

Hii ni moja ya biashara ambayo watu wengi wameipa kisogo japo wapo baadhi yao ambao wameisanukia na imekuwa ikiwatengenezea kipato cha kuendesha maisha yao.

Cha kufanya ni kwenda katika mikoa ambayo zinapatikana bidhaa za nafaka kwa wingi, mfano Mbeya kwa ajili ya kuchukua mchele na maharage kisha unasafirisha na kuleta mjini kwa ajili ya kuuza kwa jumla na rejareja, nakuhakikishia ukipata maduka angalau 20 utaweza kuingiza kwa mwezi zaidi ya Sh1 milioni.

Biashara ya mali zisizohamishika

Siku hizi watu wengi wananunua viwanja katika maeneo ambayo bado hayana watu wengi Mfano; Chanika, Vikindu, Kisemvuke na maeneo mengi kisha maeneo hayo yakianza kuchangamka, huuza viwanja hivyo kwa bei ya juu.

Huku wengine wakijenga nyumba katika maeneo hayo na kuziuza. Biashara hii ukiwa na mtaji wa kutosha inaweza kukupatia faida zaidi ya milioni moja ambayo sisi ndiyo lengo letu.

 Kulimisha mashamba kwa kutumia matrekta

Kama tunavyojua mvua sasa zinanyesha na wakulima wengi ndiyo wakati wao so unaweza kukodi trekta na kwenda nalo katika kijiji chochote ambacho watu wanalima mazao mbalimbali.

Nenda ukiwa na malengo yako kichwani kuwa kitu gani kimekupeleka, pia bei za ulimishaji ziwe rafiki kwa wakulima, naamini ukipata tenda kadhaa zinaweza kukunyanyua hapo ulipo.

Watu wengi siku hizi wamejanjaruka kwenye hili wewe ni nani mpaka uendelee kukaa nyumbani ukisubiri ajira.

 Biashara ya kuuza dagaa na samaki wakavu

Biashara hii haipishani sana na uuzaji wa bidhaa za nafaka chakufanya ni wewe kutoka ulipo na kwenda kwenye mikoa zinapopatikana dagaa kama vile Mwanza, kununua na kisha safirisha mpaka eneo unaloona linakufaa kwa biashara.

 NB: Uzuri wa biashara hizi unaweza usisafiri mara kwa mara ukizoeleka tu unaweza kuagiza mzigo kwa watu unaowaamini na ukapokea ukiwa safi kabisa. Pia biashara hizi zote unaweza kufanya matangazo mtandaoni
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags