Biashara ya uji wa mchele ilivyo na faida

Biashara ya uji wa mchele ilivyo na faida

BIASHARA YA UJI WA MCHELE ILIVYO NA FAIDA
Na Aisha Lungato
Sikukuu zimeisha maisha yanaendelea. Leo nimekuletea biashara ya uji wa Mchele. Kwa haraka unaweza kuona ni biashara ndogo lakini inaweza kuwa kubwa kwa mtu mwenye nia na maono ya kufika mbali.
Kuna msemo usemao ‘kazi ni kazi ilimaradi mkono uende kinywani’ kwa mantiki hiyo, kazi yoyote yenye kuingiza fedha kila siku unatakiwa kuifanya kwa ukubwa, kitu cha msingi ni kutafuta sehemu nzuri ambayo utapata wateja.
Mara nyingi biashara ya uji wa mchele hufanyika asubuhi na jioni huku bei yake ikianzia Sh500. Watu wengi hupatia wateja maeneo ya gereji, site za ujenzi pamoja na shule. Mtaji wake huanziaSh elfu 10.


Mahitaji
• Mchele kilo moja
• Nazi 3
• Chumvi nusu kijiko
• Sukari nusu kikombe
• Hiliki ya unga kijiko kimoja
• Pilipili mtama nusu kijiko
• Blueband (siyo laizma)
• Vikombe vya plastiki kuanzia 10
• Chupa kubwa ya vikombe 12 hata ukipata mbili siyo mbaya

Jinsi ya kupika
 Chukua mchele wako uoshe vizuri kisha uanike juani mpaka ukauke.
 Kisha chukua mchele na utwange kwenye kinu (utwange kiasi kwa ajili ya kuuvunjwa uwe vipande )
 Ukishatwanga injika sufuria yako, hakikisha sufuria ni kubwa kwani uji wa mchele una mtindo wa kuvimba
 Weka maji kwenye sufuria yako, weka hiliki, pilipili mtama, chumvi kiasi pamoja na sukari kisha weka maji vikombe vya nusu vitatu kisha acha mpaka yachemke
 Yakishachemka weka mchele wako na uache uchemke mpaka uive kabisa, ukishawiva weka tui lako la nazi la pili likikauka weka tui bubu.
 Acha tui lako la pili lichemke likiiva weka blueband yako kwa ajili ya ladha halafu anza kupakia uji wako katika chupa zako kwa ajili ya kwenda kuuza.

Angalizo uji usiufanye mzito watu hawapendi uji kama ugali hakikisha unakuwa mwepesi kiasi usiwe mwepesi sana.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post