Beyonce afunguka chanzo nywele zake kukatika

Beyonce afunguka chanzo nywele zake kukatika

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani #Beyoncé amefunguka kuwa ana changamoto ya kukatika kwa nywele zake ambapo ameweka wazi kuwa anaugonjwa wa ngozi unaofahamika kama ‘Psoriasis’.

Kwa mujibu wa Jarida la The People msanii huyo ameeleza kuwa ugonjwa huo umekuwa ukimsumbua toka mwaka 2013, na hutokana na hitilafu katika mwili wa binadamu ambapo chembe hai zinazo tengeneza ngozi zinakua haraka kuliko kawaida matokeo yake ngozi inakuwa na mabaka, ndipo nywele huanza kukatika.

Hata hivyo msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 ameeleza kuwa licha ya kupitia changamoto hizo anakumbukumbu nzuri ya nywele zake tokea akiwa mtoto namna baba yake alivyo kuwa akiziosha na kuzipaka mafuta katika saloon yao.

Mbali na hayo amesema kuwa leo Februari 20 katika onesho lake la 'Beyonce’s Formidable Fashion Evolution From Destiny’s Child’, atatoa huduma kwa watu kuosha nywele zao na kuzipaka mafuta kwa lengo la kuenzi nywele zake ya ambazo zimekuwa zikikatika siku hadi siku, tukio hilo linalofanyika jijini Texas nchini Marekani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags