Betri za simu zinazodumu na chaji miaka 53 zatengenezwa China

Betri za simu zinazodumu na chaji miaka 53 zatengenezwa China

Kampuni ya teknelojia kutoka nchini China, ‘Betavolt’ kwa mara ya kwanza imetengeneza ‘betri’ kwa ajili ya simu janja ambazo zitakuwa zikidumu na chaji kwa miaka 53 bila kuchajiwa.

 Kwa mujibu wa tovuti ya Economictimes, betri hizo zimeundwa kwa kutumia ‘kemikali’ maaulumu inayopatikana kwenye ‘isotope’ ambayo hujibadilisha kemikali kuwa umeme.

Kwa sasa ‘betri’ hizo ambazo zitakuwa za kwanza duniani zipo kwenye majaribio na ikiwa zitaonekana kufaa zitazalishwa kwa wingi ili zitumike rasmi sehemu mbalimbali.

Hata hivyo kampuni hiyo imesema mbali ya ‘betri’ hizo kutumika kwenye simu janja, pia zinaweza kutumika kwenye ‘drone’, vifaa vya kimatibabu na ‘roboti’ndogo.
.
.
.
#MwananchiScopop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags