Benzema amfungulia mashitaka waziri Darmanin

Benzema amfungulia mashitaka waziri Darmanin

Mchezaji wa ‘klabu’ ya Al-Ittihad kutoka nchini Saudi Arabia, Karim Benzema amemfungulia mashitaka Waziri wa Mambo ya Ndani Ufaransa Gerald Darmanin kwa kumchafulia jina.

Hii inakuja baada ya Benzema ku-share ujumbe kupitia ukurasa wake wa #X kuwa anaunga mkono watu wa #Gaza ambapo Darmanin kutokana na post hiyo alinukuliwa akisema kuwa Benzema anaushirikiano na kundi la Muslim Brotherhood ambalo limepigwa marufuku katika baadhi ya nchi.

Benzema alikanusha tuhuma hizo huku akieleza kuwa umaarufu wake unatumiwa vibaya katika mambo ya Siasa.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Waziri Darmanin kumshutumu Benzema, aliwahi kudai kuwa mshambuliaji huyo aligoma kuimba wimbo wa Taifa alipokuwa akijiandaa na ‘mechi’ ya ‘timu’ ya Ufaransa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags