Benzema akanusha kuwa gaidi

Benzema akanusha kuwa gaidi

Mchezaji wa ‘klabu’ ya Al Ittihad, Karim Benzema amekanusha vikali taarifa zinazosambaa kwamba yeye ni miongoni mwa watu wanaounga mkono magaidi, ikiwa ni  baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa kudai kuwa star huyo ana uhusiano na kundi la kigaidi la Muslim Brotherhood.

Kauli za kwamba Benzema anashirikiana na kundi hilo la kigaidi iliibuka baada ya star huyo kuweka wazi hisia zake kupitia mitandao ya kijamii juu ya mgogoro unaoendelea baina ya Palestina na Israel.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vinaeleza kuwa kuna taarifa zinadai baadhi ya viongozi wanataka ‘staa’ huyo apokonywe uraia wa Ufaransa huku kukiwa na ripoti pia anaweza kupokonywa hadi Tuzo ya FIFA Ballod D’or ambayo alishinda mwaka jana ikiwa atakutwa kweli na hatia ya kushirikiana na kundi hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags