Bellingham apata tuzo ya mchezaji bora wa kiume

Bellingham apata tuzo ya mchezaji bora wa kiume

Kiungo mshambuliaji wa ‘klabu’ ya #RealMadrid, #JudeBellingham usiku wa kuamkia leo amepata tuzo ya mchezaji bora wa kiume katika tuzo za ‘Laures Sports Awards’ zilizotolewa nchini Uingereza

Bellingham amekuwa mwanasoka wa kwanza mwenye umri mdogo kuchukua tuzo hiyo ya heshima ambapo alipata tuzo hiyo siku moja baada ya kufunga ‘goli’ katika dakika za lala salama ambapo Madrid waliibuka na ushindi wa bao 3-2 dhidi ya #Barcelona kwenye mashindano ya El Clasico.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa na msimu mzuri tangu ajiunge klabuni hapo mwaka 2023 akitokea Borussia Dortmund na ameweza kufunga mabao 21 katika mashindano yote.

Hadi sasa msimu huu Bellingham ambaye ana uraia wa nchini Uingereza amepata tuzo tatu mfululizo ikiwemo ya Golden Boy, Kopa Trophy na Laureus.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags