Beki wa kaizer Cheifs auawa kwa kupigwa risasi

Beki wa kaizer Cheifs auawa kwa kupigwa risasi

Beki wa Kaizer Cheifs mwenye miaka 24, Luke Fleurs ambaye alijiunga na ‘timu’ hiyo akitokea SuperSport United Oktoba mwaka jana, amepigwa risasi na kuuawa wakati wa tukio la utekaji nyara huko Honeydew.

Taarifa hiyo imethibitishwa na ‘klabu’ hiyo ambapo imeeleza kuwa Fleurs alikuwa katika kituo cha mafuta jana na ndipo walipofika watu kadhaa ambao walimtaka atoke nje ya gari lake kisha kumpiga risasi na kuondoka.

"Ni kwa huzuni kubwa tunatangaza kwamba mchezaji wa Kaizer Chiefs, Luke Fleurs alipoteza maisha jana usiku wakati wa tukio la utekaji nyara huko Johannesburg," ilisema taarifa ya klabu hiyo.

“Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia yake na marafiki katika wakati huu mgumu. SAPS inashughulikia suala hilo na maelezo zaidi yatawasilishwa kwa wakati ufaao. Roho yake mpendwa ipumzike kwa amani.”

Fleurs alianza kucheza soka la kulipwa akiwa Ubuntu Cape Town 2017, kabla ya kuhamia SuperSport United mwaka mmoja baadaye, aliondoka SuperSport mwaka jana, 2023 na kujiunga na Chiefs kama mchezaji huru.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post