Batman atunukiwa Hollywood Walk Of Fame

Batman atunukiwa Hollywood Walk Of Fame

Mhusika wa kubuni anayetambulika kama Batman rasmi ametunukiwa nyota ya heshima ya ‘Hollywood Walk of Fame’ mchana wa jana Alhamis Septemba 26, 2024.

Kwa mujibu wa Hollywood ametunukiwa heshima hiyo kufuatia uhusika wake uliochochea kukua wa teknolojia kwa zaidi ya miaka 85 pamoja na burudani iliyokuwa ikiwafurahisha watu wa jinsia zote.

Mbali na kutunukiwa nyota hiyo, wakati huo huo aliweka rekodi mpya ya kuwa muhusika wa kubuni kuingia katika kitabu cha Guinness World Record ambapo tuzo hiyo ilikabidhiwa na mwamuzi rasmi wa Guinness World Record, Michael Empric.

Nyota hiyo iliwekwa karibu na nyota ya mwanzilishi mwenza Bob Kane na muigizaji Adam West, aliyecheza kama Batman katika kipindi cha televisheni cha miaka ya 1960.Post Descriptions






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags