Bastola iliyotumiwa kwenye mauaji ya AKA yapatikana

Bastola iliyotumiwa kwenye mauaji ya AKA yapatikana

Baada ya ukimya wa muda mrefu kuhusiana na ‘kesi’ ya mauaji ya msanii kutoka South Afrika Kiernan Forbes maarufu kama AKA hatimaye bastola iliyotumika kumutoa uhai imepatikana, jeshi la polisi lathibitisha.

Kwa mujibu wa Zambia monitor news imeeleza kuwa mkuu wa polisi wa kwa-Zulu-Natal, Nhlanhla Mkhwanazi, amekataa kutoa taarifa zaidi kuhusiana siku na eneo ambayo silaha hiyo ilipatikana, kwa madai ya kuwa kufanya hivyo itaharibu uchunguzi ambao umefikia kwa usiri.

Lakini alieleza kuwa mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyeshitakiwa kwa mauaji ya msanii huyo. Ikumbukwe AKA aliuawa mwezi Februari mwaka huu nje ya mgahawa jijini Durban.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags