Barua ya Tupac kuuzwa milioni 218

Barua ya Tupac kuuzwa milioni 218

Moja ya story zinazogonga vichwa huko mitandaoni ni hii ya barua ya msanii maarufu aliyezaliwa jijini New York na kuishi California, Tupac Shakur imetangazwa kuuzwa kwa Sh Milioni 218.5.

Barua hiyo ya mapenzi ya mwaka 1995 lenye shairi la ‘All Eyes On Me’ aliloliandika kwa aliyekuwa mpenzi wake Simi imeingizwa sokoni na itauzwa kwa kiasi cha Sh. Milioni 218..

Unaambiwa kuwa Tupac alikuwa akiandika barua hizo za mapenzi na mwisho wa siku alizitolea ngoma kali zilizopendwa na kila mtu.

Wakati wa umaarufu wake hakuwa anasikizana na wasanii wenzake wa rap kutoka pwani ya mashariki akiwemo P Diddy na Notorious B.I.G.

Bali na usanii wake Tupac pia alitokea kwa filamu kadhaa ikiwemo filamu ya magenge, na filamu ya mchezo wa vikapu, Above The Rim.

Msanii huyu alifariki Septemba mwaka wa 1996 mjini Las Vegas baada ya kupigwa risasi mara nne.

Alipelekwa hospitali lakini akaaga dunia siku sita baadaye akiwa na umri wa miaka 25. Aliyemuua hajawahi kupatikana.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags