Baraka: Nimechoka kuonekana mbaya, Nafanyiwa figisu

Baraka: Nimechoka kuonekana mbaya, Nafanyiwa figisu

Msanii wa bongo fleva Barakah The Prince ameendelea kuuwasha moto kupitia mitandaa ya kijamii na leo amedai kuwa ataweka wazi figisu zote alizowahi kufanyiwa toka mwaka 2016.

Baraka kupitia ukurasa wake wa Instagram ameachia ujumbe mzito kwa kueleza kuwa leo atafichua figisu zote alizowahi kufanyiwa kwani tayari ana list na ushahidi wote.

Aidha mwanamuziki huyo ameeleza kuwa amechoshwa na kuandamwa na baadhi ya watu ambao wanania mabaya juu ya career yake.

Hayo yote ni baada ya Barakah ku-trend kutokana na tukio la kususia mahojiano aliyokuwa akifanyiwa na moja ya chombo cha habari nchini, baada ya kukasirishwa na swali la mtangazaji lililohusisha jina la Alikiba.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags