Bado hujachelewa anza mwaka na mambo haya

Bado hujachelewa anza mwaka na mambo haya

Kama ulivyo msemo wa vijana wengi mtaani kuwa mwaka mpya na mambo mapya, kama mnavyojua wiki hii na wiki inayofuata ndizo wiki ambazo watu wanarejea makazini huku wengine wakiwa wanaenda kuanza kazi katika ofisi ambayo ndiyo mara yake ya kwanza.

Leo katika segment yetu ya kazi tutakusogezea mada ambayo itakusaidia na kukutoa hapo ulipo na kufikia sehemu fulani si kwa wale tu wanaoenda kuanza kazi bali hata kwa wenyeji ambao wao hujiita makontawa kazini.

Unajua kabisa wewe umeajiriwa kwa ajili ya kazi fulani au katika kitengo fulani na hiyo kazi inakupatia tu riziki ndogo ambayo kwa maisha ya sasa hivi haiwezi kukutosha unachotakiwa kukifanya ni kuanza kuondoa hofu, wasiwasi, na kujinenea mema kila siku, kuwa unaweza kufanya jambo, huu mwaka ni wako unaitaji kuinuka na kuwa mtu wa tofauti.

Hii inaweza kuwa rahisi kutokana na wewe kuishi vizuri na watu yaani namaanisha kujichanganya na wafanyakazi wengine hii itakusiaidia kupata madini na ufahamu mpya kutoka kwa waajiriwa wengine kazini, unachotakiwa kukifanya ni…

  • ANZA KWA KUJIANDAA

Jambo kubwa la msingi ni kujiandaa kama unavyojua mwezi bado haujachanganya vizuri so anza kwa kujikubali kwanza wewe mwenyewe kuwa unaweza kufanya jambo fulani, na kama unahitaji kujifunza kuhusu kitu chochote pia inabidi uanze kuchunguza wenzio wanafanyaje na uanze kwa kufanya majaribia hata kwa siku mbili.

  • JIKUBALI

Watu wengi wanachukulia kujifunza jambo jipya kama mahojiano na polisi yaani hutakiwi kabisa kukosea, ni hivi kukosea kupo so unachotakiwa ni kufanya kwa kujiamini na kujikubali kwani hakuna anayezaliwa anajua so zingatia kujikubali, na uamini katika wewe.

  • KUJITOA

Ukiachilia mbali na kujikubali jambo jingine la msingi ni kujitoa, unapofika kazini unahitaji kujitoa kwa hali na mali, waswahili wanasema ‘Jikune unapoweza’ utakapo maliza kazi zako kama kunakazi ambazo unaweza kuzifanya nje ya hizo ulizomaliza ni kujitolea kufanya kazi nyingine hii itakusaidia hata siku kazi yako itakapopata shida labda kitengo ulichopo kikavunjwa, kwa kujitoa kwako kunaweza kukusaidia kuendelea kupata nafasi kazini kwenu.

  • KUTAFUTA KITU CHA KUFANYA NJE YA KAZI

Kauli ni moja mwaka mpya na mambo mapya, sawa unafanya kazi na unapata kipato lakini ukitoa mahitaji yako yote kiasi unachobaki nacho ni kidogo sana, so chakufanya ni kutafuta biashara nje ya mshahara wako ambayo itakuingizia kipata hata kama siyo kikubwa bali pesa iingie.

Kutegemea sehemu uliyopo kuwa ni mkombozi wa maisha yako haiwezi ikawa kweli, Stephen Wasira aliwahi kusema “Mshahara hauwezi ukamfanya mtu atajirike, mtu analipwa mshahara kwa ajili ya kula tu’’ hivyo basi tafuta biashara ambayo itakuingizia kipato nje ya kazi unayofanya.

  • ACHA KUFUATA MIKUMBO

Leo nimekumbuka mbali sana hili neno walimu wengi walikuwa wanatusihi kuacha kufuata mikumbo, ni vile vile kwako ulienda kazini mwenyewe na maisha ya nyumbani kwako/kwenu wewe ndiye unayajua kwa hiyo akili kichwani mwako fanya kilicho kupeleka acha kufuata mienendo ya watu ambao wana zaidi ya miaka 10 kazini kwa sababu watu hao watakupotosha.

Ukweli mchungu wengi ambao wanamuda mrefu kazini wanapenda sana kuwapotosha wafanyakazi wapya ili nawao waweze kuharibika kama wao so na wewe ukifuata mkumbo unaweza ukafukuzwa kazi na wenzio ukawaacha hapo hapo, achana na mikumbo ya ajabu fanya kazi kwa bidii usiangalie watu wanasema nini.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post