Babu Tale: Naamini naandaliwa mke mzuri wakuja kulea wanangu

Babu Tale: Naamini naandaliwa mke mzuri wakuja kulea wanangu

Duuuuuuh! Kuna binadamu wanapitia magumua sana katika haya maisha, basi bwana yule Mbunge wa morogoro ambae pia ni meneja wa msanii maarufu ndani na nje ya nchi Diamond, Babu Tale ameweka ujumbe mzito katika ukurasa wake wa instagrama na kuandika kuwa.

“Najua wengi wenu mtajiuliza huyu mwengine ni nani..? Sababu hao watatu sura zao sio ngeni sana machoni mwenu..huyo mgeni kwenu anaitwa ZAHID.. nimwanangu pia.. kama ilivyo hao watatu.. Huyu nae nimempoteza mamayake miez miwili iliyopita” ameandika Babu Tale

Aidha aliendelea kutoa yamoyoni kwa kuandika hivi  “ sina budi kumshukuru Mungu kwakila Mtihani anaonipa..kwamaana anaamini nitauweza... siwezi tena kulia,zaidi nakuomba uendelee kunifungulia riziki kila uchwao.. na naamini unaniandalia Mama yao mpya (mke mzuri) wakuja kuwalea nakuwaongoza Kwenye misingi mizuri yakumjua Mungu” ameandika Mh. Babu Tale

Unakipi cha kumshauri Mh. Tale, dondosha komenti yako hapo chini mfuatiliaji wetu wa Mwananchi Scoop.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags