Babu Tale: Miaka 2 chozi la upendo

Babu Tale: Miaka 2 chozi la upendo

Kutoka kwenye ukurasa wa Babu tale ameeandika ujumbe huu mahususi kwa Hayati mke wake toka alipoiaga dunia ni miaka miwili sasa.

'Miaka 2 ya chozi la upendo.

Leo tarehe 28 Juni, 2022 natimiza miaka miwili pasina uwepo wako Shammy wangu.

Moyo wangu umezungukwa na kumbukumbu za upendo zinaamsha maumivu ambayo siwezi kuyabadili na kuwa furaha, lakini imani imejijenga kuwa Mola hakosei.

Namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kukupumzisha mahala pema Mkewangu Kipenzi, Rafiki na Mshirika wangu wa maisha.

Mimi nipo imara na nasimamia misingi ya kile tulichopigania kwa pamoja na mambo yanakwenda vizuri kwa uwezo wake Mungu.

Dada TT na Kaka zake wote wako salama na Mimi bado moyo wangu umesimama juu ya kuamua kwenye mapenzi, kwa kifupi sina mpenzi mpaka leo.

Najua unajua kuwa kwa hili gubu langu...ndio kabisaaa, naweza rushiwa sufuria ya maharage....

Naendelea kukulelea Watoto wako vizuriiiiii, nao Mwenyezi Mungu anawabariki kwa upendo usiopimika.

Endelea kupumzika Kwa amani Mama TT.

upendo wako umenasa kila mjongeo wa moyo wangu.'






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags