Baba yake Mohbad adai kutishiwa maisha na mkwewe

Baba yake Mohbad adai kutishiwa maisha na mkwewe

Baba wa marehemu mwanamuziki Mohbad kutoka nchini Nigeria kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni ameeleza kuwa aliyekuwa mke wa Mohbad, Wunmi na wakili wake wanatishia kumuua.

Baba Mohbad, Joseph Aloba ameweka wazi suala hilo wakati akizungumzia kuhusiana na kuchelewa kwa majibu ya vipimo vya mwili wa mwanaye pamoja na DNA na kueleza kuwa alipigiwa simu ya vitisho na #Wunmi ambapo amedai kuwa amerekodi kila kitu.

Ikumbukwe kuwa Marehemu Mohbad alifariki Septemba 12, 2023 Ikorodu nchini Nigeria.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags