Baba wa Mohbad: Waliozaa na mwanangu wajitokeze

Baba wa Mohbad: Waliozaa na mwanangu wajitokeze

Baba mzazi wa marehemu mwanamuziki Mohbad, Joseph Aloba ametoa wito kwa wanawake ambao waliwahi kuzaa na Mohbad wajitokeze.

Aloba ameyasema hayo kupitia video aliyoichapisha kwenye mtandao wa TikTok akidai kuwa mwanamke yeyote mwenye mtoto wa Mohbad na ambaye yuko tayari kufanya DNA ili kuthitisha ajitokeze.

“Mwanamke yeyote duniani ambaye ana mtoto kwa Mohbad tafadhali ajitokeze sasa. Itakuwa furaha kubwa kwangu kujua kwamba mwanangu Mohbad aliacha watoto, Tunachohitaji kufanya ni uchunguzi wa DNA," amesema.

Hii inakuja baada ya mjane wa Mohbad aliyefahamika kwa jina la Wunmi kukataa kufanya DNA ili kuthibitisha kuwa Liam, ni mtoto wa Mohbad kutokana na kuwepo kwa uvumi huwenda mtoto huyo siyo wa msanii huyo.

Ikumbukwe kuwa Mohbad alifariki Septemba 12, mwaka 2023, mjini Lagos, akiwa na umri wa miaka 27.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags