Baba wa bilionea Elon Musk asema hajivunii mwanae

Baba wa bilionea Elon Musk asema hajivunii mwanae

Wakati watu wengi wanatamani kuwa na watoto wenye akili na mabilionea, hiyo sio kwa baba wa Tajiri wa kwanza duniani kwa sasa, Elon Musk.

Baba wa nguli huyo ambaye ni CEO wa kampuni ya Tesla, anejulikana kwa jina la Errol Musk, amesema kuwa yeye hajivunii kabisa kuwa baba wa Elon wala Elon kuwa bilionea pekee kwa sababu familia nzima ya Musk imepata mambo ya ajabu. Kulingana na yeye, kwa kweli, Mkuu wa Tesla na SpaceX hajafurahishwa na maendeleo yake ya kazi.

Errol Musk mwenye umri wa miaka 76 alisema hayo kwenye kipindi cha Australia ‘The Kyle and Jackie O Show.’

Wakati wa mahojiano hayo yaliyochukua dakika 20, aligusia mambo mbalimbali, Pia hata watoto aliozaa na binti yake wa kambo.

Haya bwana... ungekuwa una mtoto tajiri kama Elon na wewe usingejivunia mafanikio yake?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags