Baada ya ndoa yao kuvunjika, Atakiwa kulipa zaidi ya sh 20 milioni kila mwezi

Baada ya ndoa yao kuvunjika, Atakiwa kulipa zaidi ya sh 20 milioni kila mwezi

Mwigizaji wa Marekani Halle Berry na Olivier Martinez ambaye pia ni muigizaji kutoka Ufarasa ambao walikuwa ni wanandoa hatimaye ndoa yao imevunjika rasmi.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2013 na baada ya miaka mitatu walitengana bila kupeana taraka, huku katika ndoa yao wakiwa wamepata mtoto wa kiume anayefahamika kwa jina la Maceo, baada ya miaka saba sasa tangu kutengana wamefikia muafaka wa kutalakiana kisheria.

Talaka hiyo inaenda sambamba na makubaliano kuwa Olivier atalazimika kutoa $8,000 ambayo ni zaidi  tsh 20 milioni kila mwezi kwa ajili ya malezi ya mtoto wao.

Huku kwenye upande mwingine wa malezi Berry atakuwa na haki ya kumlea mwanaye kuanzia Jumatatu hadi Jumatano, huku Martinez atamlea Jumatano hadi Ijumaa.

.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags