Baada ya miezi tisa meli ya kitalii yakamilisha safari yake

Baada ya miezi tisa meli ya kitalii yakamilisha safari yake

Baada ya miezi tisa baharini, meli kubwa zaidi duniani iitwayo ‘Royal Caribbean’s Icon of the Seas’ imemaliza safari yake huku ikitarajiwa kurejea Miami siku chache zijazo.

Meli hiyo iliyoanza Safari zake jijini Miami nchini Marekani Januari 27 mwaka huu imeripotiwa kumaliza safari yake kwa wateja wao wa awamu ya kwanza ambapo imefanikiwa kutembelea nchi 65 pamoja na mabara saba.

Bei ya abiria wa kima cha chini kabisa kwa mtu mmoja ilianzia $1,820 ambayo ni zaidi Sh 4 milioni, kwa siku saba Icon Seas ina jumla ya vyumba 2805 na inauwezo wa kuchukua abiria 7,600.

"Icon of the Seas", inasehemu kwa ajili ya familia, bustani, sehemu ya kuogelea, club na sehemu nyingine nyingi za kula bata. meli hii imetengenezwa na Royal Caribbean International, matengenezo yake yalianza mwaka 2016 jijini Finland.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags