Baada ya miaka mitano P Square wamerudi na balaa zito

Baada ya miaka mitano P Square wamerudi na balaa zito

Alooooh!Mambo ni moto na mazuri kwa mashabiki na wapenzi wa muziki baada ya wakali wa hit songs kutengana kwa miaka mitano na kuamua kurudisha kundi lao tena, yes ni wale wale mapacha maarufu P-square wamerudi tena na balaa zito.

P-Square ambao ni wanamuziki kutoka nchini Nigeria wamerudi na balaa zito katika mziki na kufanikiwa kuingia kwenye orodha ya wasanii ambao wamewahi kuujaza ukumbi wa Royal Albert Hall uliopo London, nchini Uingereza.

Mapacha hao wanaungana na wasanii wengine wakubwa kama The Beatles, Adele, Elton John, Wizkid, Miriam Makeba, David Gilmour, ambao wamewahi kuuza tiketi zote za ukumbi huo uliopo London wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 5,272 tu pia katika tamasha hilo waliweza kuimba nyimbo zao za zamani .

What your comment kuhusiana na comeback ya mapacha hao?







Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags