Baada ya Beatrice zamu ya Salama, kujibiwa na Rais Samia

Baada ya Beatrice zamu ya Salama, kujibiwa na Rais Samia

Ikiwa imepita siku moja tuu tangu mbunifu wa mavazi Beatrice Mwalingo, kujibuwa ‘komenti’ na Rais Samia Suluhu Hassan, sasa ni zamu ya Mtangazaji Salama Jabir, ambapo alimuomba Rais Samia kufanya naye mahojiano, katika siku yake ya kuzaliwa.

Rais Samia kupitia ukurasa wake wa X (twitter) alimjibu Salama kwa kueleza kuwa angependa kufanya mahojiano naye lakini wajukuu na wadogo zake wengine tayari wamemuwahi hivyo basi Mungu akipenda ombi hilo litatimizwa kwenye Birthday ya mwakani 2025.

Licha ya hayo Rais Samia alimualika kwenda kula keki pamoja kwenye Birthday ya mwaka huu kwa niaba ya wote waliomtumia salamu za kheri.

Ikumbukwe kuwa Leo Januari 27, ni siku ya kuzaliwa ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo anatimiza miaka 64.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags