Baa zungusha kama tulivyo, nyumbani njaa kali

Baa zungusha kama tulivyo, nyumbani njaa kali

#Weekend ndiyo hii wazee wa kujirusha siku yenu imefika, wengi wanatafuta pesa lakini kichwani wamejiwekea malengo ya kumwagilia moyo mwishoni mwa wiki, shida siyo kutumia pesa, tatizo ni kwa wale wanaotafuta wakizipata wanasahau kutumia na familia zao, hapa nazungumzia wazee wa zungusha kama tulivyo, siyo vibaya kutumia na marafiki lakini ni viziri kuanza na familia.

Kuna baadhi ya watu wanapenda kupewa heshima 'baa', kwa kutoa 'ofa' za soda na bia huku nyama choma zikiwa zimeja mezani lakini ukichunguza kiundani kwenye familia zao lazima uchoke, si ajabu kusikia familia haijala nyama mwezi mzima au kunywa soda ni siku kuu kwa siku kuu lakini baba au mama kutwa kuweka heshima 'baa' na washikaji.

Marafiki ni muhimu lakini familia ni muhimu zaidi, ni jambo zuri kama familia yako itaanza kufurahi nyumbani kabla hujuaenda kufurahisha watu kwenye kumbi za starehe, watoto hupata furaha zaidi wakipewa vitu vidogo kama zawadi au kupelekwa kwenye michezo yao, kuliko hata hao unaoenda kuwanunulia 'bia' ambao wakilewa hawachelewi kukutukana bila kujali kuwa hela ya kulewea umetoa wewe, lakini ukifurahisha familia yako ni rahisi kupata baraka kwa kidogo ulichowapatia

Siyo lazima kutoka unaweza kutumia weekend kukaa nyumbani na familia yako, kuna baadhi ya watoto kumuona mzazi ni ndoto za Bunuasini kwao, ukiuliza sababu kubwa ni kwamba mzazi anatoka mapema na kurudi usiku watoto wakiwa wamelala, kuwa makini na hao unaoenda kutumia nao #Weekend hii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags