Azindua manukato yaitwayo talaka baada ya kuacha na mumewe

Azindua manukato yaitwayo talaka baada ya kuacha na mumewe

Binti wa mfalme kutoka Dubai Princess Mahra bint Mohammed bin Rashid Al Maktoum, ameripotiwa kuzindua manukato yaitwayo ‘Divorce’ (Talaka) baada ya kuachana na mumewe Julai mwaka huu.

Kwa mujibu wa baadhi ya vyombo vya habari vinaeleza kuwa baada ya ukimya wa miezi kadhaa, Princess Mahra amerudi tena kwa kishindo na kutangaza uzinduzi wa manukato yake mapya katika mitandao ya kijamii yaliyozua gumzo kwa baadhi ya watu.

Kufuatia na hilo maoni ya watu mbalimbali wanaendeleza kuwa huwenda Mahra hakuachana na mumewe na kuwa alitaka tu attention kutoka kwa watu kufuatia na bidhaa yake hiyo mpya inayotarajiwa kuingia sokoni siku chache zijazo.

Utakumbuka kuwa mwezi Julai mwaka huu mtoto wa mfalme huyo aliingia kwenye vichwa habari baada ya kutangaza kuachana na mumewe Mana al-Maktoum katika mitandao ya kijamii kwa kumuacha kwa talaka tatu.

“Mume wangu mpendwa, kwa kuwa umejishughulisha na marafiki wengine, natangaza rasmi talaka yetu. Nakupa talaka, nakupa talaka, na nakupa talaka, kuwa makini. Mkeo wa zamani,” aliandika Princess Mahra






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags