Azarenka atangaza kupumzika tennis

Azarenka atangaza kupumzika tennis

Nyota wa tennis kutoka nchini Belarus Victoria Azarenka ametangaza kupumzika kidogo kwenye mchezo huo kutokana na matatizo binafsi ya kifamilia huku akitupwa nje ya michuano ya Miami Open 2022 na kinda kutoka Jamhuri ya Czech Linda Fruhvirtova mwenye umri wa miaka 16.

Azarenka ambaye alitwaa ubingwa wa Australian Open mwaka 2012 na 2013 alipoteza kwa seti 6-2 na 3-0 huku hii ikiwa ni mara ya pili kwa nyota huyo kuchukua mapumziko kama ilivyokuwa  msimu 2016/17 baada ya kutengana na mzazi mwenzie kisha kurejea tena kwenye tennis mwaka 2018.

" Wiki mbili zilizopita sikuwa sawa kutokana na matatizo binafsi ya kifamilia ndio maana mchezo uliopita nilitumia muda mwingi kucheza na kushinda lakini kwa sasa nataka kuchukua likizo na nitarejea baadae kidogo” amesema Azarenka






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags