Azam yawekewa mkwanja mrefu kuiua Yanga

Azam yawekewa mkwanja mrefu kuiua Yanga

‘Klabu’ ya Azam FC leo Jumatatu itakuwa mgeni wa ‘timu’ ya #Yanga kwenye mchezo wa ‘Ligi’ kuu mzunguko wa sita ‘mechi’ itakayochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na tayari ‘mastaa’ wa Chamazi wametengewa kitita cha fedha mezani kama watashinda ‘mechi’ hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti limepenyezewa na mmoja wa viongozi wa juu wa Azam (jina tunalo), tajiri wa kikosi hicho Yusuph Bakhresa ametenga zaidi ya Tsh 500 milioni kwa ‘timu’ hiyo kama itaifunga Yanga.

“Miongoni mwa ‘mechi’ muhimu kwetu ni pamoja na hii ya Yanga. Tunataka kushinda ili kuendelea kukaa juu kwenye msimamo.

“Na nikuambie, kila mtu ndani ya ‘timu’ anaitaka ‘mechi’ hii, tajiri tayari ameahidi zaidi ya Sh 500 milioni kwa wachezaji na ‘benchi’ la ufundi kama tutashinda, unaona ni ‘mechi’ rahisi?” amesema kiungozi huyo.

Hata hivyo, Azam imekuwa ikikutana na ugumu dhidi ya Yanga katika ‘mechi’ tano Wanachamazi hao wameambulia ‘sare’ moja tu na kufungwa mara nne.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na alama 13 baada ya ‘mechi’ tano, huku Yanga ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 12 na nafasi ya kwanza ipo Simba yenye alama 15 baada ya michezo mitano.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags