Ayra starr: Nimepata umaarufu nikiwa na umri mdogo

Ayra starr: Nimepata umaarufu nikiwa na umri mdogo

Nyota wa Afrobeats kutoka nchini Nigeria Ayra Starr, amejigamba kwa kudai kuwa amepata umaarufu katika muziki akiwa na umri mdogo.

Msanii huyo ameyasema hayo akiwa katika mahojiano na ‘Music Talks’ amedai kuwa amepata umaarufu akiwa bado mdogo baada ya kutoa EP yake ya kwanza ya '19 & Dangerous' mwaka 2021.

“Ep yangu ya kwanza ilivuma barani Afrika na nilizidiwa kukua mbele ya kila mtu nikiwa bado nina umri mdogo. Tunahitaji kuruhusu wasanii kukua na kujikuta, hivyo sijui hata kama hii ndiyo fomu yangu ya mwisho

Watu tofauti kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanapenda muziki wangu. Sauti yangu ni ya kipekee." amesema

Hata hivyo amesema kuwa kuna zama na nyakati bora zaidi kwake akidai siku za usoni anaweza kuwa mkubwa zaidi kwa Afrika katika masuala ya muziki.

Pia amefichua kuwa aliwahi kurekodi nyimbo tano mara ya kwanza alipokutana na  Don Jazzy, ambaye baadaye alimtia saini Mavin Records.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 22 amewahi kufanya wimbo kama Commas, Sability, No Love, Rash na nyengine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags