Ayra Starr aomba radhi kutomsalimia mama Burna Boy

Ayra Starr aomba radhi kutomsalimia mama Burna Boy

Baada ya wadau wa muziki kuchukizwa na kitendo cha msanii kutoka nchini Nigeria Ayra Starr kumpita Meneja na mama mzazi wa Burna Boy, Bi Bose Ogulu bila kumsalimia wakati wa sherehe za Afrozons Pre-Grammy party iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Royal Box Event Center, jijini Lagos, hatimaye Ayra ameomba msamaha kuhusiana na tukio hilo.



Ayra kupitia ukurasa wake wa X ameomba radhi kwa Mama Burna Boy na mashabiki na kwa kumtafasiri vibaya kwani hakuwahi kuwa msichana mbaya wa kukosa heshima ya kusalimia, huku akiweka wazi kuwa alirudi kumsalimia kila mtu vizuri.

Licha ya hayo mama Burna Boy alitunukiwa Tuzo ya heshima kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kumpambania kijana wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags