Mwanaharakati wa mazingira na mwanafunzi wa misitu kutoka nchini Ghana aitwaye Abubakar Tahiru (29) ameweka rekodi mpya ya dunia kwa kukumbatia miti 1,123, ndani ya saa moja.
Jaribio lake la kuweka rekodi lilifanyika katika msitu wa kitaifa wa Tuskegee pamoja na misitu minne ya Kimataifa katika jimbo la Alabama nchini Marekani ambapo kwa mujibu kwa mitandano ya kijamii ya Guinness Tahiru anaingia katika kitabu cha ‘Guinness World Records’ kwa kuwa mtu wa kwanza kumiliki rekodi hiyo.
Kufuatia na mahojiano yake aliyoyafanya baada ya kumaliza Tahiru ameeleza ugumu aliyokumbana nao ambapo alidai kuwa ugumu ulikuwa ni kutoka mti mmoja hadi kwenda mti mwingine.
Baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza ya utaalam wa misitu katika moja ya vyuo vikuu vya juu vya Ghana, Abubakar alihamia Alabama, Marekani, mwaka jana ili kuanza shahada yake ya uzamili katika misitu Chuo Kikuu cha Auburn, ambapo hapo ndipo alipopata wazo la kutaka kuweka rekodi hiyo ya dunia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply