Avunja rekodi ya kupika kwa saa 199

Avunja rekodi ya kupika kwa saa 199

Baada ya mpishi kutoka nchini #Nigeria, #HildaBaci kuvunja ‘rekodi’ ya dunia ya Guinness kwa kupika siku nne mfululizo (saa 100) hatimaye ‘rekodi’ hiyo imevunjwa na #AlanFisher kutoka #Ireland kwa kupika saa 199 na dakika 57.

Kwa mijibu wa  Guiness World Records kupitia ukurasa wake wa X wame-share taarifa hiyo Leo Jumanne, Novemba, 7 kwa kueleza kuwa ‘rekodi’ ya  mpishi kutoka Nigeria Hilda Baci imevunjwa na Alan Fisher, kutoka Ireland aliyepika kwa muda wa saa199 na dakika 57 katika mgahawa mmoja nchini #Japan.

#AlanFisher anadaiwa amevunja ‘Rekodi’ mbili za Dunia za Guinness moja ikiwa kupika kwa muda mrefu na nyingine ni kuoka mikate kwa muda mrefu ambapo alitumia muda wa saa 119 na dakika 57 kupika na saa 47 na dakika 21 kwa kuoka mikate.

Huku vyombo vya habari nchini humo vikieleza kuwa Fisher alichukua zaidi ya saa 160 jikoni.

Hilda Baci alitangazwa rasmi kuvunja ‘rekodi’ na Guiness World Records mwezi Mei mwaka huu baada ya kupika vyakula tofauti tofauti kwa saa 100 bila ya kupumzika.
.
.
.
#






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags