Avunja rekodi kwa kutengeneza wigi refu zaidi duniani

Avunja rekodi kwa kutengeneza wigi refu zaidi duniani

Mtengenezaji mawigi kutoka Lagos nchini Nigeria, Helen Williams amevunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa kutengeneza 'wigi' refu zaidi duniani kwa kutumia mikono.

Kwa mijibu wa Guiness World Records kupitia ukurasa wao wa X wame-share taarifa hiyo na kueleza kuwa Helen amevunja rekodi mpya ya kutengeneza wigi refu zaidi duniani kwa kutumia mikono, lenye urefu wa mita 351.28 (1,152 ft 5).

Aidha Hellen kufuatia mahojiano yake na vyombo vya habari ametoa uzoefu wake katika utengenezaji na kueleza kuwa alitumia siku 11 tu kufanikisha kutengeneza 'wigi' hilo.

Huku gharama alizotumia zikiwa ni dola 2,493 ambapo alinunulia vifaa mbalimbali ikiwemo vifurushi vya nywele bandia 1,000, spry za nywele makopo 12, gundi 35 na vipande vya mawigi 6,250.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudkaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags