Mwanamume mmoja kutoka Poland aitwaye Łukasz Szpunar (53) amevunja rekodi na kuingia katika kitabu cha ‘Guinness World Records’ kwa kukaa kwenye barafu zaidi ya saa 4.
Szpunar amekuwa mwanaume wa kwanza kukaa kwenye sanduku la vipande vya barafu kwa saa 4 na dakika 2 huku akiipita rekodi ya awali kwa dakika 50.
Haya siyo mashindano ya kwanza kwa Szpunar alikuwa mshindi wa pili katika mashindano ya Walrus ya Poland, ambapo alikaa kwa zaidi ya saa nne kwenye beseni la maji baridi.
Hapo awali rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Wim “The Iceman” Hof kutoka Uholanzi ambapo alikaa kwenye barafu kwa saa 1 na dakika 53 rekodi iliyowekwa mwaka 2013.
Ikumbukwe kuwa mwanamke wa kwanza kuweka rekodi ya kukaa kwenye barafu kwa muda mrefu anatoka nchini Poland ambapo aliingia kwenye kitabu cha ‘Guinness World Records’ kwa kukaa ndani ya barafu kwa saa 3 dakika 6 na sekunde 45, mwanamke huyop alijelikana kwa jina Katarzyna Jakubowska (48).
Leave a Reply