Atumia wimbo wa Davido kupiga mkwanja

Atumia wimbo wa Davido kupiga mkwanja

Kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii Bongo kutikisa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ngoma za wasanii wengine kwa kuzifanyia cover, ndivyo ilivyotokea kwa kijana kutoka nchini Nigeria, Emmanuel Ogbole, maarufu kama Emzy Pondeck

Emzy amejipatia umaarufu mkubwa unaomfanya apige pesa ndefu kwa kufanya 'show' ya cover ya wimbo uitwao 'Kante' wa mwanamuziki Davido ambao upo kwenye albamu yake ya Timeless.

Kibogo bongo pia wapo wasanii ambao walianza kufuatiliwa baada ya kuanza kufanyia cover nyimbo za wasanii maarufu, kati ya wasanii hao wakiwemo Dayoo, Anjela.

"Kante' ni wimbo wa kumi kati ya nyimbo 16, kwenye albamu ya Davido iitwayo 'Timeless' iliyotoka mwaka 2023, huku nyingine zikiwemo 'Over Dem', 'Godfather', 'Unavailable' na 'Away'. Hadi sasa wimbo huo kwenye YouTube channel ya Davido unawatazamaji  milioni 6 ukiwa na miezi tisa tangu utoke.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags