Atishia kubeba mabomu akiwa juu ya bembea

Atishia kubeba mabomu akiwa juu ya bembea

Mwanaume mmoja ambaye hajafahamika jina hadi  sasa, amedakwa na polisi baada ya kuwatishia watu waliokuwa kwenye bembea la Ferris katika hifadhi maarufu ya Santa Monica, California kuwa amebeba ‘bomu’ kwenye ‘begi’ lake.

Tukio hilo liliotokea jana jioni katika kivutio cha watalii, ambapo mwanaume huyo aliwaambia watu walioko katika bembea la kuzunguka kuwa amebeba ‘bomu’ huku akiendelea kuwasogelea watu wao.

Idara ya Polisi ya Santa Monica inasema mtu huyo alipanda bembea hilo huku akiwafokea maafisa lakini hawakuweza kuelewa alichokuwa akisema alipokuwa akining'inia katikati ya bembea.

Kutokana na hayo bembea hilo lilisimamiswa na juhudi za kuwatoa watu walioko ndani zilifanyika na jeshi la zimamoto, na hatimaye, kijana huyo alikamatwa na baada ya upekuzi polisi wanasema hawakukuta mabomu yoyote kwenye begi lake kama alivyokuwa akidai.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags