Atengeneza ndege inayofanya kazi kama baiskeli

Atengeneza ndege inayofanya kazi kama baiskeli

Mwanafunzi mmoja aitwaye Fusha Sakai kutoka Chuo Kikuu cha Umma cha Osaka kilichopo nchini Japani, ameibua hisia za wengi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutengeneza na kuonekana akiwa katika majaribio ya ndege yake inayofanya kazi kama Baiskeli.

Ndege hiyo iliyopewa jina la ‘Tsurugi’ mwendeshaji anatakiwa kunyonga kama vile unavyoendesha baiskeli kwa ajili ya kuipa nguvu ya kupaa angani zaidi na kukufanya kuendelea na safari yako.

Kupitia video hiyo inayosambaa mitandaoni ilirekodiwa kuwa ilitembea kwa umbali wa kilomita 19, huku baadhi ya wadau mbalimbali walitoa maoni yao ambapo walieleza kuwa kufuatiwa na ubunifu huo ndoto za watu kumiliki ndege binafsi zinakalibia kuwa kweli.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post