Atembea na cheti kuthibitisha umri wake

Atembea na cheti kuthibitisha umri wake

Mwanaume mmoja kutoka nchini #Urusi aliyefahamika kwa jina la Dennis Vashurin mwenye umri wa miaka 36 imemlazimu kutembea na cheti chake cha kuzaliwa kwasababu ya kuthibitisha umri wake.

Kwa mujibu wa Mirror News inaeleza kuwa kijana huyo licha ya kuwa na umri mkubwa lakini watu humuona kama mtoto mwenye umri wa miaka 14 kwasababu ya kuwa na mwili mdogo na sura yake kutozeeka kutokana na matatizo ya kiafya.

Lakini baadhi ya watu wameshinndwa kumuamini nchini humo hivyo inamlazimu kutembea na cheti mtaani kama uthibitisho wa umri wake katika jamii inayo mzunguka

Denis alipata umaarufu miaka miwili iliyopita baada ya kuhojiwa na mmoja ya chombo cha habari nchini humo kuhusu mwonekano wake, na watu wamekuwa wakivutiwa na wengine kumdhihaki lakini bado hajaonesha kukata tamaa kutokana na hali yake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags