Atembea kama Miss kwenye mazishi ya rafiki yake

Atembea kama Miss kwenye mazishi ya rafiki yake

Mwanamitindo kutoka nchini Marekani Erica L. Carrington amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutembea kama miss katika mazishi ya mbunifu mwenzake Vernest Moore wakati wa kuaga mwili.

Kufuatia mahojiano yake jana Jumanne na TMZ mrembo huyo amedai kuwa amefanya hivyo kwa sababu marehemu rafiki yake angependa iwe hivyo huku akidai kuwa hajuti kufanya hivyo japo ameumizwa sana na msiba huo.

Kutoka na jambo hilo baadhi ya watu waliohudhuria katika mazishi hayo walikosoa wazo la Erica huku wengine wakifurahishwa na kitendo hicho kwa kuwa alivaa moja ya mavazi yaliyotengenezwa na marehemu Vernest.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags