Atakayetumia VPN bila kibali kukiona cha mtema kuni

Atakayetumia VPN bila kibali kukiona cha mtema kuni

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), imepiga marufuku matumizi ya mtandao binafsi(VPN) isipokuwa kwa kibali maalum.

Taarifa ya katazo hilo imetolewa jana Oktoba 13,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA.

Taarifa hiyo ilisomeka "Kwa kuzingatia kanuni ya 16(2) ya kanuni ya mwasiliano ya kielektroniki na Posta kuhusu maudhui mtandaoni ya mwaka 2020, mtu hatatoa hatamiliki na hatasambaza teknolojia, programu tumizi au kitu chochote kinachoendana na ambacho kinaruhusu au kumsaidia mtumiaji kupata maudhui yaliyokatazwa.

"Kwa kuwa TCRA imebaini upatikanaji wa maudhui yaliyokatazwa kwa kupitia matumizi ya mtandao binafsi(VPN) kinyume cha kanuni.

"Hivyo tunautaarifu umma kuwa kampuni ambayo kwa asili ya majukumu na kazi zao,matumizi ya VPN hayazuiliki,kutoa taarifa kwa TCRA juu ya VPN wanazotumia na taarifa zote muhimu ikiwemo anuani ya itifaki ya mtandao(IP Adress) kabla ya ya Oktoba 30,2023," imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa TCRA itaendelea kuchukua hatua kudhibiti matumizi ya VPN yasiyo halali ikiwemo kuzuia upatikanaji wa ambazo haijatolewa taarifa au kusajiliwa.

"TCRA inaukumbusha umma kuwa utoaji ,umiliki au usambazaji wa teknolojia ,programu,programu tumizi au kitu chochote kinachoendana na ambaco kinaruhusu au kusaidia mtumiaji kupata maudhui yaliyokatazwa ni kosa la jinai.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kosa kwa anayekutwa na hatia ya matumizi ya VPN ni Sh5 milioni au kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post