ASMA JAMIDA: Mabinti hawapewi heshima kwenye ucheshi

ASMA JAMIDA: Mabinti hawapewi heshima kwenye ucheshi

Jina: Asma Majid (Jamida)

Birthday: September 27th

Alooooooh!! Mwananchi Scoop this furahi day bwana tumemmulika binti ambaye anafanya sanaa ya ucheshi, Asma Jamida. Bila shaka sio jina geni kwako na kama ulikua unamfahamu juujuu tu, nikukaribishe uweze kumfahamu kindakindaki sasa.

Binti huyu Asma ni Stand-Up Comedian akiwa chini ya platform ya Cheka Tu.

Asma Jamida ni binti mwenye umri mdogo lakini mambo anayoyafanya kwenye tasnia ya ucheshi ni makubwa. Tuanzie hapa bwana ambapo alianza kujulikana kwenye jamii kupitia video yake ya ucheshi iliyoelezea maisha ya wanyama akielezea, “je binadamu tungekua tunaishi maisha kama ya wanyama ingekuaje?”

Hata hivyo, binti huyo ana elimu ya Diploma in Mass media and Communication aliyoipata kutoka Chuo cha The Arusha East Africa Training Institute.

 Ukiachana na hayo bwana, Asma alishawahi kutunukiwa tuzo ya heshima kama msichana ambaye anafanya stand-Up comedy kwa ajili ya kuwainspire wengine ambao wanahisi kama ni jambo gumu kufanya kazi ya ucheshi.

Licha ya hayo yote bado Asma anaeleza changamoto mbalimbali ambazo anakumbana nazo wakati akiwa anafanya kazi yake ya ucheshi ambapo moja kati ya mengi ni hili hapa;

“Binafsi napitia changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni kutopewa thamani kama binti kwamba nafanya ucheshi, thamani bado haijawa kubwa sana katika sanaa ya ucheshi hususan kwa mabinti,” alisema.

Aliongea pia kwakusema, “Unakuta mtu unaperform lakini wakati huohuo mtu mawazo yake anakuwa anawaza kitu kingine kabisaa, wala hazingatii lile unalolifanya.”

Mbali na mitihani au misukosuko hiyo, bado Asma ana matarajio makubwa katika sanaa hiyo na ana tamani kufika mbali zaidi na kuhakikisha iwe tasnia ambayo inakubalika zaidi kwenye jamii.

Nikukumbushe na hili pia ambapo Asma amezaliwa jijini Mwanza, hospitali ya Bugando, akiwa mtoto wa pili aliyefanikiwa kusoma elimu yake ya msingi katika shule ya Songambele na sekondari Kirumba na Alharamain, jijini dar es salaam na hatimaye akafanikiwa kupata chuo Arusha.

Anachokipenda na Asichokipenda Asma

“Kitu ambacho sikipendi kwenye maisha yangu ,sipendi kudharaulika, sipendi umasikini lakini vitu ambavyo navikubali napenda kucheka, kuongea na watu lakini sipendi watu ambao ni wabinafsi,” alisema mwanadada huyo.

Kitu usichokifahamu kuhusu Asma

Aloooooh!!! Hivi ulikua unafahamu kama huyu binti ni mtoto wa kihayaa? Kupitia mahojiano yetu alifunguka na kusema kuwa yeye ni Muhaya tena originali kabisaaa.

Kuhusu masuala ya mahusiano

Asma alifunguka kuwa hayuko kwenye mahusiano yaani yuko Single in short. Hahahahah ila kasema ataangalia huko mbeleni kama itafaa kuwa kwenye mahusiano au la.

Chochote unachotaka watu wakijue kuhusu wewe

“Napenda watu wafahamu kuwa mimi ni muandishi wa habari na ni mtangazaji mzuri pia.”

Historia ya Asma kwenye sanaa ya ucheshi ilianzia akiwa chuoni na role model wake alikuwa Marehemu Boss Martha. Huyo ndiyo mtu aliyemvutia zaidi kwenye ucheshi.

Her new project

Project yake mpya ambayo anatarajia kuitoa siku za hivi karibuni ni kuhusiana kutoa content tofauti tofauti zitakazokuwa zinakwenda kupitia Instagram pamoja na YouTube.

We appreciate Asma because she is a girl who believes in fighting for the better success in life and career so she can inspire other girls in the society.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags