Ashtakiwa kwa kuuza viungo vya miili ya wafu

Ashtakiwa kwa kuuza viungo vya miili ya wafu

Meneja wa chumba cha kuhifadhia maiti cha shule ya mafunzo ya kitabibu ya Harvard Medical School, bwana Cedric Lodge nchini Marekani, na wengine watatu wameshtakiwa kwa kununua na kuuza viungo vya mabaki ya binadamu.

Lodge akishirikiana na mke wake Deniz anadaiwa alichukua vichwa, ubongo, ngozi na mifupa kutoka kwa maiti zilizotolewa kwa shule ya matibabu ya chuo kikuu hicho na kuviuza mtandaoni.

Waendesha mashtaka wanasema Lodge alitumia wadhifa wake kama meneja wa mpango wa ‘Anatomical Gifts Program’ katika Shule hiyo ya matibabu kwa kukataa akisema maiti zilizotolewa kwa ajili ya utafiti wa matibabu.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags