Ashinda taji la Miss Universe akiwa na miaka 60

Ashinda taji la Miss Universe akiwa na miaka 60

Mwanamke mmoja kutoka nchini Argentina anayefahamika kwa jina la Alejandra Rodriquez, amezua gumzo mitandaoni baada kushiriki mashindano ya Miss Universe akiwa na miaka 60 na kufanikiwa kupata ushindi.

Inaelezwa kuwa hapo awali umri wa washiriki wa Miss Universe nchini humo ulitakiwa kuwa kati ya miaka 18 hadi 28 na kigezo kingine ilitakiwa mshiriki asiwe na mtoto lakini sheria hizo zilibadilishwa mwaka jana.

Pamoja na umri wake kuwa mkubwa mwanamke huyo bado anaonekana mrembo mithili ya binti wa miaka 18.

Alejandra amesema siri ya mwonekano huo ni kuwa na maisha yenye afya, kula vizuri, kufunga mara kwa mara na kufanya mazoezi ya viungo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags