Ashika rekodi ya kuwa na nywele ndefu masikioni

Ashika rekodi ya kuwa na nywele ndefu masikioni

Aliyekuwa mwalimu mkuu katika shule ya Madurai nchini India, Anthony Victor ndiye mtu pekee anayeshikilia rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa nywele ndefu zaidi za masikio duniani.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zimeeleza kuwa mwalimu huyo mstaafu ana nywele zinazochipuka kutoka katikati ya masikio yake sehemu ya nje ambazo zina urefu wa sentimita 18.1

Victor anatajwa kudumu katika rekodi hiyo bila mpinzani kwa zaidi ya mika 15 na mpaka sasa hakuna mtu ambaye amewahi kukuza nywele za masikio tangu yeye aliposhika rekodi hiyo mwaka 2007 hivyo kumfanya kuwa na nafasi kubwa katika kitabu cha rekodi ya dunia ya Guinness cha mwaka 2023.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags