Asha Baraka amtaka Wema Sepetu aolewe

Asha Baraka amtaka Wema Sepetu aolewe

Mkurugenzi wa Twanga pepeta, Asha Baraka amevunja ukimya kwa The Tanzanian Sweetheart, Wema Sepetu kuhusiana na suala la mrembo huyo kuwa na mahusinao mapya kila siku.

Kupitia mahojiano yake na Wema, kwenye kipindi cha Cook with Wema Sepetu, kinachoongozwa Chimama, Asha Baraka amefunguka na kusema “Mimi namwambia  Wema kuwa nataka kucheza harusi kabla sijafa, nimechoka kila siku Wema ana mahusiano tuu”

“Ushakuwa na wanaume chungu nzima sasa imefikia wakati basi, kubali hata kuolewa uke wenza na uache kuchagua wewe ni mtoto wa kiislamu”

Kwa upande wa Chimama, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Chakula kilikuwa kitamu sana sema ilibaki kidogo kinitokee puani…Nakupenda ivyo ivyo Mama yangu”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags