ASAP afunguka kwa mashabiki ujio album mpya ya Rihanna

ASAP afunguka kwa mashabiki ujio album mpya ya Rihanna

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani #ASAPRock amefunguka mbele ya mashabiki juu ya ujio wa Album mpya ya mpenzi wake #Rihanna baada ya kuulizwa na mashabiki nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa Daily Mail News inaeleza kuwa mashabiki walimuuliza ‘rapa’ huyo kuhusu muziki wa Rihanna na Album yake ya tisa baada ya kutokea katika onesho la wapendanao mjini Paris nchini humo.

Hata hivyo ASAP aliwaeleza mashabiki hao kuwa muda si mrefu Rihanna atatoa album yake mpya na hivi sasa anaifanyia kazi kwa kuandaa nyimbo zitakazo sisimua nyoyo za mashabiki wake.

 Ikumbukwe kuwa albamu ya mwisho ya Rihanna amabayo ilifahamika kama ‘Anti’, ilitolewa mwaka wa 2016 na ilijumuisha nyimbo kama vile ‘Work’ akimshirikisha Drake, ‘Kiss It Better’,  ‘Needed Me,’ na ‘Love on the Brain’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags